Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru anawatangazia wananchi wote kuwa tarehe 25 Aprili 2018 ni siku ya maadhimisho ya wiki ya chanjo mbalimbali na katika siku hiyo uzinduzi ngazi ya Halmashauri wa chanjo mpya ya kinga ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV) utafanyika.

Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya chanjo mpya ya kinga ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV) yatakayofanyika katika Hospitali ya wilaya Meru ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Aidha mratibu wa chanjo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Jonathan Mollel ametoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto wao kwenye Zahanati na Vituo vya Afya vilivyopo kwenye maeneo yao  ili waweze kupata chanjo ya kinga ya saratani ya mlango wa kizazi inayotolewa kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 kuanzia saa 03:00 asubuhi kwani hiyo ni salama na imedhibitishwa na shirika la afya Duniani (WHO).

Aidha mratibu mollel amefafanua kuwa chanjo zote zitatolewa kwenye Zahanati na vituo vya Afya kuanzia saa 3:00 asubuhi pia vyandarua vya mbu vitatolewa kwani tarehe 25 Aprili kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa Malaria duniani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: