Sunday, 15 April 2018

United kutafuta ushindi wa 6 mfululizo kwa West Brom hii leo

Steve Wilson kocha wa West Brom amewaonya wachezaji wake kuhusu aina ya timu ambayo wanakwenda kuikabili, Wilson amekumbushia wachezaji wake kuhusu kile United walichofanya Etihad wiki iliyopita.
Katika mechi 9 ambazo West Bromich wamekutana na Manchester United, wameshinda michezo 3 tu huku wakipoteza michezo 4 kati ya hiyo na kwenda suluhu katika michezo 2.
Tayari Jose Mourinho amewapa United alama 71 idadi ambayo haijawahi kufikiwa tangu Sir Alex Ferguson aiache United, kama leo United watashinda mchezo wao baasi watakuwa wamefikisha alama 74.
Lakini West Bromich Albion sio wabovu sana haswa wanapokwenda katika dimba la Old Traford, katika michezo yao 3 ambayo wameifunga Manchester United michezo 2 wameshinda katika dimba la Old Traford.
Mchezo huu una kumbukumbu kubwa kwa mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, katika mechi ya mwisho ya Ferguson katika dimba la OT alikutana na WBA ambapo walitoka sare ya bao 5-5 na Lukaku aliifungia WestBromich hattrick.
West Bromich wana rekodi mbovu sana katika viwanja vya ugenini, katika mechi zao 15 za mwisho walizocheza ugenini, wamepoteza michezo 11 na kutoka sare katika michezo yao minne ugenini.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: