Mjumbe wa chama cha mpira wa kikapu Arusha Bw.Bariki Kilimb7a ameeleza adha wanayoipata kutokana na  ukosefu wa kiwanja cha kufanyia mazoezi na kuchezea mpira wa kikapu jijini Arusha.

Akizungumza na Msumbanews Blog Bw.Bariki amesema kuwa chama cha mpira wa kikapu Arusha kiliwapeleka baadhi ya wadau kwenda kusoma Uganda na Nairobi nia ikiwa ni kuwafundisha watoto na vijana.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa ukosefu wa kiwanja hicho cha mpira wa kikapu kunawaathiri kwa kiasi kikubwa kwani walikuwa wakitegemea kiwanja cha Soweto lakini kwa sasa wamezuiliwa kwa muda kwa ajili ya usalama zaidi kwani  kuna makazi ya watu katika eneo hilo.

Aidha ameendelea kusema wameshindwa kufanya ligi ya mkoa ambapo walitegemea kupeleka timu ya mkoa kushindana jijini Dar-es-salaam lakini imeshindikana kutokana na ukosefu wa kiwanja cha kufanya mazoezi

Amehitimisha kwa kusema kuwa chama cha mpira wa kikapu hakihitaji fedha kutoka serikalini kwa sababu wana wafadhili hivyo wameiomba serikali kuwapatia eneo la wazi kwa lengo la kujenga kiwanja cha mpira wa kikapu ili kukuza vipaji vya watoto na vijana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: