Spika wa Bunge, Job Ndugai amewatahadharisha wabunge wanaokusudia kupeleka hoja binafsi kuacha kutafuta umaarufu mitandaoni badala yake wafuate kanuni za bunge.

Ndugai ameyasema hayo leo Aprili 12 na kumtaja mbunge wa Nzega mjini, Hussein Bashe kuwa ni mfano wa wabunge hao ambao hutoa taarifa ya kusudio la kupeleka hoja binafsi lakini ghafla wanaanza kutangaza hoja zao mitandaoni.

"Wabunge wengine nawashauri mfuate kanuni na mfano ni Bashe, mnataka umaarufu tu wakati mnatakiwa kufanya lobbying (ushawishi) kwanza ili hoja zenu ziungwe mkono." amesema Ndugai.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: