Tuesday, 10 April 2018

Singida United yataka kulipiza kisasi

Klabu ya Singida United imeweka wazi kuwa wanatamani kukutana na Mtibwa Sugar kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho nchini ili waweze kuwafunga na kupata nafasi ya kuwakilisha nchi kimataifa.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga ameweka wazi kuwa mchezo huo umepita lakini wanatamani kukutana na Mtibwa kwenye hatua ya fainali endapo watafuzu kwenye nusu fainali.

“Tumepoteza mchezo muhimu dhidi ya Mtibwa, na ni kwamara ya kwanza tumekubali kufungwa Uwanja wa nyumbani lakini yameshapita na tunamsubiri kwenye FA kama tutafanikiwa kuingia wote fainali tutawaonesha,” amesema.

Aidha Sanga ameongeza kuwa kwasasa timu hiyo minajipanga na mchezo wao ujao wa ligi kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa jumatano hii kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Wakati huohuo Sanga amekanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa kuwa klabu hiyo imeshindwa kuwalipa mishahara wachezaji wake wa Kimataifa ambapo amesema wachezaji wote wapo kambini na wamelipwa stahiki zao zote.

No comments:

Post a comment