Monday, 23 April 2018

Singida United wapewa utaratibu na TFF

 Baada ya leo asubuhi klabu ya Singida United kutangaza kutoa fursa kwa mashabiki wake kuingia bure kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili Kombe la Shirikisho, TFF imetoa utaratibu unaotakiwa kufuatwa.

Shirikisho hilo la soka nchini limeeleza kuwa utaratibu utafuatwa kama kawaida ambapo tiketi za mchezo zitauzwa kulingana na uwezo wa uwanja, lakini Singida United wamezinunua zote hivyo mashabiki watapewa tiketi ndio waingie uwanjani.

Singida United kesho watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida kuwania nafasi ya kucheza fainali ya Kombe la shirikisho na Mtibwa Sugar ambayo tayari imefuzu baada ya kuifunga Stand United.

TFF imewatoa shaka mashabiki na wapenda soka wote kuwa mamlaka na wadau wote wanaohusika na mchezo huo, wamekubaliana na Singida United kulipa gharama za tiketi zote ambazo ni makadilio ya uwezo wa uwanja wa Namfua.

No comments:

Post a comment