Monday, 9 April 2018

SERIKALI YASHAURIWA KUTOTUMIA MAWAKALA KATIKA KUSIMAMIA RASILIMALI ZA TAIFA.


Na: Mdau wa maendeleo, Arusha 

Wachambuzi nguli wa masuala ya Siasa na Uchumi Duniani na Afrika nzima wamepongeza hatua ya Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli Kwa hatua kadhaa anazozichukua katika kulinda, kutetea na Kupigania Raslimali za Taifa la Tanzania.

 Wakimtaja kuwa Dr. John Pombe Magufuli ni Rais namba Moja  mzalendo WA kweli Afrika.

Ukweli wa mambo unajidhihirisha katika muonekano wa Jamii na Famili zilizozungukwa na Rasilimami hizo mashuhuri Ulimwenguni zikiwa katika hali ya umasikini na ufukara mkubwa Kwa muda mrefu. 

Hii ni dhahili shahiri kuwa Rasilimali za Taifa hili zimekuwa zikiibiwa, kusombwa na kudhurumu haki ya msingi ya  watanzania kwa miaka mingi Sana. "watanzania Tumeibiwa Sana!!!!!! ,Hata hii Tanzanite Kama ingekuwa ya kuisha basi Leo yangekuwa yamebaki mashimo matupu!!!!. 

Wengi walibeza na kukejeli ahadi na Maagizo aliyokuwa akiyatoa Mh. Rais kwa Serikali yake, Wengine walithubutu kusema "Hawezi"nk,nk.Mh.Rais alitoa maagizo ya kujegwa ukuta wa kuzunguka machimbo ya mererani ndani ya muda wa Miezi Sita (Six month). Kwa shauku kubwa na uzalendo wa majeshi yetu na uongozi wa Mkoa wa Manyara kuunga mkono Maelekezo ya Rais ili Rasilimali zetu zisiibiwe hovyo hovyo, Ukuta huo ulikamilika kwa miezi mitatu. (Three month time). Hii ni kazi nzuri ya kujivunia.Na hongera Sana Sana Mkuu wa Mkoa wa  Manyara na Majeshi yetu yote kwa kazi nzuri kwa manufaa ya watanzania takribani Million  60. 

Ghalama zilizotumika kujenga Ukuta Wa kulinda Madini Adimu Duniani ulighalimu kiasi cha 5.Billion and something.Thamani hii ni sawa na Grams either moja au  Mbili za Tanzanite.Sasa watanzania tujiulize ni Magrams mangapi yalishatoroshwa,Kuibwa na kudhurumu haki ya watanzania, ?Na ni grams ngapi ambazo serikali hii imeziokoa zisiibiwe ili kila mtanzania anufaike na keki ya Rasilimali zetu. Kukamilika kwa uzio WA ukuta ni adhima ya mtanzania kunufaika na Rasilimali za nchi.

Aidha kwa dhati Kabisa, Ningependa kuipongeza sana serikali ya Tanzania ya awamu ya Tano katika kuhakikisha Rasilimali za nchi yetu ni zetu kikwelikweli na ziwanufaishe watanzania kikwelikweli. watanzania tunafaa kujivunia haya na kutembea kifua mberee na kujivunia utanzania Wetu.Nilipenda Sana kuishauri serikali ya Awamu ya Tano ya Dr. John Pombe Magufuli kufanya yafuatayo ili kufikia malengo ya kulinda, kutetea na kusimamia Rasilimali za nchi kwa manufaa ya Taifa.

Sasa ni wakati wa Serikali kusimamia na kuendesha uchimbaji, uzalishaji ,Ugawaji na Uuzaji wa Rasilimali za nchi. Mataifa yote Duniani, yenye Rasilimali Kama madini, Gesi,Mafuta nk, Yanasimamia yenyewe(Serikali ndiye watch Dog wa mwenendo wa uchakataji, uchimbaji, uhifadhi na uuzaji wa Rasilimali husika.) Hii,itasaidia kupunguza na kuondoa ubadurifu, katika sekta hizo muhimu kwa taifa.Tumejenga Ukuta, Tumeweka ulinzi nk, nk,Lakini bila usimamizi wa Serikali katika uchimbaji na Processing ya Madini  hayo bado hakika tutakuwa tunarudi kule kule. 

Aidha Maeneo yote, yenye Rasilimali za nchi, Asiwekwe WAKALA yaani (Agent) Kusimamia ama kuendesha shughuli za Rasilimali zinazovunwa. Kuwepo na Sara na sheria ambazo serikali ndiyo atakuwa muhusika mkuu yaani ,na sio Mshiriki tu,Endapo serikali itasimamia yenyewe hakika Uchakataji, Uzalishaji, utunzanji, usambazaji na uuzaji wa Maliasili zetu utakuwa mzuri, Wenye faida kwa Watanzania na Taifa kwa Ujumla. 

Viwanja vyetu vya ndege vya kimataifa viboreshwe na, Visimamiwe na kuendeshwa na Serikali kuu. Hii itasaidia kudhibiti mapato ambayo nafikiri yangetumika katika kuwapelekea watanzania miradi ya Maendeleo. Kwa muda mrefu sana serikali imekuwa ikitumia neno (WAKALA).wakala wa mbegu, wakala wa pembejeo za kilimo,nk,nk.Naishauri serikali kuu yenyewe ndio iwe WAKALA. and( not third part Distributor).

Nia njema na thabiti ya Serikali ya Mh.Dr.John Pombe Magufuli inatakiwa kuungwa mkono na wananchi wote kwa kufanya kazi halali kwa bidii ili Taifa linapopata maendeleo, Maendeleo hayo yaendane na dhana ya kumkwamua mwananchi katika Dimbwi la umasikini. Athari za Wananchi asipofanya kazi ni kuwa, Serikali itafanya juhudi zake zote za kimaendeleo lakini Mwananchi asiyefanya kazi hawezi faidi Wala kupata maendeleo.Tusitegemee kuwa IPO siku maendeleo ya mwananchi yanapatikana kwa kugawiwa fedha za bure na Serikali. No thank you. Hayo sio maedeleo. Maendeleo yanakwenda sambamba na kufanya kazi kwa vidii. (watanzania tuchape kazi)

MWISHO nipende kusisitiza na kuwakumbusha watanzania wote kuwa Msingi na Nguzo Pekee ya kufanikisha ndoto, Adhima na Maono ya Mh. Rais wetu mpendwa wa kuifanya Tanzania kuwa na Uchumi bora Duniani ni kuilinda, kuidumisha Amani,Upendo na Mshikamano wa Taifa letu. Maendeleo yanapatika kwenye Taifa lililo na Amani,Upendo na Mshikamano miongoni mwa Wananchi na Serikali yao.Na wajibu wa kuitunza Amani ya Taifa letu ni yetu sote watanzania.(Mimi & wewe).Kuna Baadhi ya Viongozi wa kisiasa wamekuwa wakitumia Lugha za kichochezi,lugha ya kuudhi,na kujalibu kuikatisha tamaa Serikali hii.Hawa Tuwabeze na kuwapinga kwa nguvu zetu zote. Tusiwape nafasi katika Jamii zetu, Tusiwape nafasi Katika Fikra zetu. 

" Watanzania kazi yetu ni Moja KUCHAPA KAZI "

Asanteni sana

Netho Ndilito
(Hard Working  & God  Fearing Servant)

No comments:

Post a comment