Monday, 23 April 2018

Serengeti Boys watinga Nusu Fainali CECAFA U17

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imepata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Sudan katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA U17 inayoendelea nchini Burundi.

Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inakwenda Nusu Fainali ya michuano hiyo kutoka Kundi B, ikiungana na Uganda, zote zikiwa na pointi nne kila moja, wakati Sudan inaaga baada ya kupoteza mechi zote mbili.

Zanzibar ni timu nyingine iliyopangwa katika kundi hilo, lakini iliondolewa kwa kuwasili na wachezaji waliozidi umri.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Muyinga mjini Bujumbura, mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Alphonce Msanga mawili dakika za nne na 59, Mustapha Nankunku dakika ya 27, Edson Mshirakandi dakika ya 28, Jaffar Mtoo dakika ya 78 na Kelvin Paul dakika ya 83.

Mechi yake ya kwanza, Aprili 15, mwaka huu Serengeti Boys ilitoa sare ya 1-1 na Uganda

No comments:

Post a comment