Tuesday, 3 April 2018

Rais Magufuli amteua Mkemia Mkuu wa Serikali mpya


Rais John Magufuli amemteua Dk Fidelice Mafumiko  kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huo wa Dk Mafumiko umeanza  Jumanne Aprili 3, 2018.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,  Gerson Msigwa imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Dk Mafumiko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

Dk Mafumiko anachukua nafasi ya Profesa Samuel Manyele ambaye amemaliza muda wake.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: