Saturday, 14 April 2018

Okwi amuandikia ujumbe wa shukrani Naibu Spika Dr. Tulia

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi amemshukuru Dr. Tulia Ackson kwa kumpa nafasi ya kuwa miongoni mwa mabalozi wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon 2018.
Video Player
Kupitia mitandao yake ya kijamii ya Instagram, Twitter na Facebook, Okwi ameandika ujumbe wa kumshukuru Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Tulia Ackson kwa kumpa nafasi ya kuwa miongoni mwa mabalozi wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon 2018.
Nina furaha kubwa sana kuwa mwanafamilia wa Mbeya Tulia Marathon 2018, Binafsi napenda kushukuru Tulia Trust kwa kunipa nafasi ya kuwa Miongoni mwa mabalozi wa Mbio hizi kushirikiana nao katika kuboresha miundombinu ya Elimu na Afya na nitakuwepo kushiriki na ninyi hapo Mei 6 2018.
Ujumbe wa Emmanuel Okwi kupitia mtandao wake wa Kijamii wa Isntagram
Ujumbe wa Emmanuel Okwi kupitia mtandao wake wa Kijamii wa Twitter
Ujumbe wa Emmanuel Okwi kupitia mtandao wake wa Kijamii wa Facebook
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: