Wednesday, 18 April 2018

Nuh Mziwanda adai kitendo alichokifanya Diamond sio cha kiungwanaMsanii wa muziki, Nuh Mziwanda amedai kitendo alichokifanya Diamond sio cha kiungwana kwani wanawake wote ni kama mama zetu hivyo tunapaswa kuwaheshimu.

Muimbaji huyo amesema hayo muda mchache baada ya rais huyo wa WCB kuachia video akishikana shikana na wanawake wawili tofauti.

Tayari Diamond ameshahojiwa na jeshi la polisi na wamedai watamchukulia hatua za kisheria muimbaji huyo wakimkuta na hatia.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: