Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia.
BUNGE la kumi na moja limeanza leo Aprili 3 ambapo Naibu Spika, Tulia Ackson, amewaapisha wabunge wawili, Dkt. Godwin Mollel wa Siha na Maulid Mtulia wa Kinondoni.

Wabunge hao wameapishwa kufuatia uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha na Kinondoni,  ambapo wabunge hao walihamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mtulia, alikuwa mbunge wa Kinondoni kupitia Chama cha Wananchi  (CUF), kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena jimbo hilokupitia chama hicho.  Mollel, alikuwa mbunge wa Siha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) kabla ya kujiunga na CCM.

Hata hivyo,  kiapo hicho hakikushuhudiwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ambao hawakuwepo katika kikao hicho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: