Friday, 20 April 2018

Mtibwa sasa yazisubiri Singida na JKT Tanzania


Klabu ya soka ya Mtibwa Sugar imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho nchini baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Stand United kwenye mchezo wa nusu fainali uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 yote yakifungwa na Hassan Dilunga na kutinga fainali itakayopigwa Juni 2, mwaka huu katika dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Baada ya kufuzu fainali leo, Mtibwa sasa inamsubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Singida United na JKT Tanzania katika nusu fainali ya pili itakayopigwa April 23, mwaka huu.
Kwenye ligi msimu huu Mtibwa Sugar, inashika nafasi ya 6 ikiwa na alama 33 baada ya mechi 24. Wakati Stand United ambao wamepoteza nusu fainali ya leo ipo nafasi ya 9 ikiwa na alama 28.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: