Tuesday, 10 April 2018

Mlinzi wa Floyd Mayweather apigwa risasi

Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa mtu mmoja anaedaiwa kuwa mmoja wa walinzi wa karibu wa bondia wa Marekani, Floyd Mayweather amepigwa risasi nje ya Hoteli ya Atlanta hapo jana asubuhi siku ya Jumatatu.
Mtandao wa habari za michezo wa TMZ Sports umeripoti kuwa kwamujibu wa taarifa za Polisi, risasi imetoka kwa mtu ambaye alikuwa kati ya moja ya magari matatu yaliyokuwa yamewasili nyuma ya hoteli ya InterContinental Buckhead majira ya saa 3 a.m. asubuhi siku ya Jumatatu.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha CNN kimeripoti kuwa mlinzi huyo ambaye jina lake halija fahamika amefikishwa kwenye Hospitali ya Grady Memorial kwaajili ya kupatiwa matibabu kufuatia risasi hiyo kumjeruhi mguuni na hali yake inaendelea vizuri.
Taarifa kutoka Polisi zinaeleza kuwa wanaamini bondia, Mayweather alikuwa sehemu ya msafara huo uliyoshambuliwa licha ya kutokuwa na uhakika kama yeye ndiye alikuwa mlengwa wa tukio hilo.

No comments:

Post a comment