MAMBO 21 YALIYOJIRI KWA MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA ATHUMANI KIHAMIA NA MADIWANI WA JIJI HILO TANGU ATUE JULAI 2016

1. Julai 2016 alifuta posho za madiwani za simu na mafuta shs 250,000/=kwa mwezi kwa kila diwani.

2. Agosti 2016 alipunguza posho za ukaguzi wa miradi toka shs 100,000/= hadi shs 50,000/ nauli ikiwa shs10,000/= toka shs 60,000/=.

3. Mkurugenzi alikataa kusaini mikataba ya maduka ya stendi ndogo kwa kuwa haikufuata taratibu huku madiwani na mbunge wa Godbles Lema wakimtaka kusaini hiyo mikataba.

4.Oktoba 2016 baraza la madiwani  walijigeuza kama kamati ili kumkataa mkurugenzi huyo kwa tuhuma za kutekeleza maagizo yao yakiwemo ya kutomsimamisha kazi mtendaji wa kata ya Murieti.

5.Oktoba 2016 mtandao wa jamii forum ulitumiwa na madiwani kutoa taarifa kuwa mkurugenzi huyo ameondoka na shs milioni 500 za jengo la utawala la halmashauri ya Kaliua alipokuwa mkurugenzi mtendaji.

6. Novemba 2016 wanasiasa hao walimtengenezea kashfa ya kumteka mwalimu Batuli Kisaka  wa shule ya msingi Unga ltd iliyopo jijini Arusha(ambaye alijiteka).

7. Novemba 2016 mtandao wa jamii forum uliandika kuwa mkurugenzi huyo alikataa kuhojiwa na polisi kwa tuhuma za kumteka mwalimu Batuli Kisaya aliyesimamiwa kwa karibu na madiwani wa kata za Unga ltd, Meya, Levolosi na Ngarenaro.

8. Novemba 2016 kupitia mtandao wa jamii forum madiwani walimtuhumu mkurugenzi huyo kuwa ametumia mafuta lita 1900 kwa mwezi huo kwa ofisi ya mkurugenzi.

9. Novemba 2016 madiwani katika kikao cha kamati ya fedha na utawala walimtaka mkurugenzi kutoa maelezo ya maandishi kwa kupunguza watumishi 66 wa mikataba bila ridhaa yao


9. Desemba 2016 kikao cja baraza la madiwani kilivunjika baada ya kumtuhumu mkurugenzi huyo kutekeleza mambo anayoyataka badala ya maazimio yao.

10. Januari 2017 madiwani waliunda timu ya watu 5 kumshughulikia mkurugenzi huyo, ambao ni Meya Kalisti Lazaro, Ali Bananga, Efatha Nanyaro, Doita Harry, na Jenifer Mollel. Waliandaa waraka wenye tuhuma 15 na kuuwasilishaTAMISEMI.

11. Januari 2017 madiwani walojiorodhesha  na kusaini kufikia 28 kati ya 34 kumkataa mkurugenzi kwa tuhuma za kuwalipa madeni walimu 171 shs 169 milioni bila kibali chao.

11. Februari 2017 TAMISEMI iliunda tume ya watu 5 waliofika Arusha kuchunguza tuhuma 15 za mkurugenzi wa jiji  la Arusha.

12. Februari 2017 kikao cha baraza la madiwani kilivunjika baada ya kutokea vurugu kufuatia madiwani na mkurugenzi huyo kutofautiana katika hoja ya utoaji wa tenda ya maduka ya stendi ndogo hadi kiliporudiwa chini ya usimamizi wa katibu tawala mkoa Richard Kwitega.

13. Machi 2017 mkurugenzi huyo alifuta kampuni 2 ya vifaa vya ofisi na ya huduma ya chakula kwa jiji zinazomilikiwa na madiwani.

14. April 2017 diwani wa Levolosi Efatha Nanyaro alihamasisha wananchi wa jiji la Arusha kupitia ukrasa wake wa facebook kujiorodhesha hadi watimie 100,000 ili wamkatae mkurugenzi kwa tuhuma za ubabe.

15. Mei 2017 mkurugenzi huyo alikata posho za wenyeviti wa mitaa kwa kutofanya vikao vya kisheria kila robo mwaka katika mitaa yao hali iliyoongeza joto la malumbano kati ya madiwani na mkurugenzi huyo.

16. Mei 2017 mkurugenzi huyo alitoa waraka kwa wakuu wa idara na vitengo kutotoa taarifa yoyote kwa madiwani bila kibali chake kwa madai kuea yeye ndiye msemaji mkuu wa halmashauri hali iliyozua hisia hasi kwa mbunge Lema na madiwani.

17. Mei 2017 mkurugenzi aliwapigisha kura watumishi wa makao makuu akitafuta anaetoa siri za ofisi kwa madiwani ambapo mbunge na madiwani walilalamikia sana hali hiyo.

20. Juni 2017 mbunge Lema katika mkutano wa hadhara mara tu baada ya kutoka gerezani alitangaza kutomtambua  mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa kwa kudai wanakula njama kuuvuruga upinzani kwa kuingilia maamuzi ya halmashauri kupitia kwa mkurugenzi wa jiji.

VIKAO VILIKUWA VIKIFANYIKA CHINI YA ULINZI WA POLISI. KWA SASA HALI HIYO HAIPO TENA KWA KUWA HAKUNA JARIBIO  HATA MOJA LA MADIWANI  DHIDI YA MKURUGENZI KIHAMIA LILILOFANIKIWA.

Wiki ijayo tutatoa mwendelezo wa makala nyingine za jiji hili la Arusha ili kujua mapito yake. Nimeamua kuja na makala hizi ili wananchi waone jinsi viongozi wetu wanavyopata shida kutekeleza ilani ya ccm.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: