Monday, 30 April 2018

Mama Salma Kikwete ashusha wosia mzito kwa Alikiba na mkewe

Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete amewaasa wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba na mdogo wake Abdu Kiba kuwa wawe waaminifu kwenye maisha yao ya ndoa hasa hasa kwenye masuala ya simu.
Mama Salma Kikwete akiwaasa jambo Alikiba na mkewe
Mama Salma ametoa wosia huo jana Aprili 29, 2018 katika hoteli ya Serena  jijini Dar es salaam kwenye sherehe za harusi ya Alikiba na mdogo wake Abdukiba ambao wote wamefunga ndoa wiki mbili zilizopita.
Simu mtihani na ni hatari, mkiendekeza simu mnachukua mnaangalia mtaaachana kabla ya siku si nyingi. Aminianeni mkiaminiana  maisha yatakuwa mazuri, laikini kila dakika ukirudi basi umerudi unaanza kupakua nani ametuma meseji, hapana. Wakati mwingine simu inalia ikishalia ile simu unakosa amani ya moyo unatoka nje au unaingia chooni kuongea,“amesema Mama Salma Kikwete.
Kwa upande mwingine Mama Salma Kikwete amesema yeye tangu afunge ndoa na Mzee Kikwete wamekuwa wakichangia simu na mara nyingine hata kupokeleana pale inapokuwa inaita.
Alikiba na mdogo wake Abdukiba wamefunga ndoa wiki mbili zilizopita ambapo Alikiba alifunga ndoa na mchumba wake Aminah Khalef jijini Mombasa.

No comments:

Post a Comment