Wednesday, 4 April 2018

Mahakama Kutoa Maamuzi Kesi ya Wema Sepetu April 23


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 23, 2018 itatoa uamuzi kama Wema Sepetu  na wenzake wawili kama wana kesi ya kijibu au la.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka na kuufunga ushahidi wao.

Machi 23, 2018 upande wa utetezi uliwasilisha hoja katika Mahakama hiyo ili waone washtakiwa hao hawana kesi ya kujibu.

Mbali na Wema, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
 
Inadaiwa  kuwa  Februari 4, 2017 katika makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Wema anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya  aina ya bangi.

No comments:

Post a comment