Tuesday, 24 April 2018

KUBENEA ADAI HUENDA BOMBARDIER ZIKAKAMATWA TENA


MBUNGE wa Ubungo – Dar es Salaam, Saed Kubenea akichangia hoja bungeni leo kuhusu Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano inayosimamiwa na Profesa Makame Mbarawa, ameomba ufafanuzi kutoka kwa Waziri Mbarawa akidai juu ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limefunguliwa kesi, London nchini Uingereza kutokana na deni la Tsh. Bilioni 80 hali ambayo amedai inaweza kusababisha ndege za Bombadier kukamatwa.

Hayo amesema leo Bungeni, Aprili 24, 2018, na kuongeza kuwa Waziri wa katiba na Sheria anafahamua suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali anafahamu, Asha Rose Migilo na viongozi wengine wanajua, tayari Serikali ya Tanzania imelipa malipo ya awali kwa mawakili kwa ajili ya kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment