Monday, 30 April 2018

KOCHA MFARANSA SIMBA AZUIA KAMBI HOTELI YA NYOTA TANO DAR


KATIKA kupunguza pre­sha ya mechi ya watani wa jadi Yanga, Kocha Mkuu wa Simba Mfaran­sa, Pierre Lechantre am­ezuia kambi ya moja ya hoteli kubwa ya nyota tano iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Kambi hiyo ilikuwa ya maandalizi ya mechi ya watani wa jadi wa Simba na Yanga iliyotarajiwa kupigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Cham­pioni Jumatatu, kocha huyo alizuia kambi hiyo ya hoteli kubwa baada ya uongozi wa timu hiyo kupendekeza kuipeleka huko kabla ya kwenda kwenye hoteli yao wa­nayokaa kila mara iliyopo Mbezi Beach.

Mtoa taarifa huyo alisema, kikubwa kocha huyo alitaka wachezaji wake waione me­chi hiyo ya kawaida kama zilivyo mechi nyingine walizo­cheza awali.

“Uongozi wetu ulipanga timu ifikie kwenye moja ya ho­teli kubwa ya nyota tano (jina tunalo tunalihifadhi) wakati timu inatoka Morogoro ilipoweka kambi ya mechi dhidi ya Yanga.

“Lakini tulipomta­arifu kocha, alikataa kabisa na kuuomba uongozi kuiweka timu kwenye kambi yao waliyoizoea ambayo kila siku tumekuwa tukiweka kwa ajili ya maan­dalizi.

“Na kikubwa kocha alitaka kuwaweka sawa kisaikolojia kwa kuwataka waione ni mechi ya kawaida kwa maana timu ukiiweka kambini kwenye hoteli kubwa kutawafanya wa­chezaji wacheze kwa presha kubwa,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa kocha huyo kuzungumzia hilo alisema: “Nina­taka wachezaji wangu waione mechi hii kuwa ya kawaida tofauti na mashabiki wana­vyofikiria.

“Kwa sababu kama timu ukiweka kambi kwenye ho­teli kubwa wataiona mechi kubwa na presha kuongezeka kitu ambacho sikukitaka na ndiyo maana nimependekeza tufikie kwenye hoteli hiyo tuli­yoizoea.”

No comments:

Post a Comment