Wednesday, 11 April 2018

Katibu Mkuu Yanga atupiwa lawama kuondoka kwa Lwandamina

Taarifa zinazoelezwa ndani ya Yanga baada ya Kocha George Lwandamina kuondoka klabuni hapo na kurejea Zesco United, ni kutokuwa na mahusiano mazuri baina yake na Katibu Mkuu wa timu, Charles Boniface Mkwasa.

Inasemekana kuwa Lwandamina hakuwa ana maelewano mazuri na Mkwasa haswa katika masuala ya utendaji wa klabu hivyo inatajwa ikawa sababu ya yeye kuondoka na kutimkia kwa Zambia.

Zipo taarifa za chini ya kapeti zinazosema Mkwasa alikuwa akihitaji kuchukua nafasi yake ya ukocha na aachane na wadhifa wa Ukatibu Mkuu alionao kwa sasa.

Kuafuatia hayo yote kutokea, Katibu Mkuu wa Mashindano ya Yanga, Samuel Lukumay, amesema Kamati ya Utendaji itakaa baada ya mchezo wa leo dhidi ya Singida kutoa tamko rasmi kama klabu kuhusiana na kuondoka kwa Lwandamina.

Lwandamina ameondoka Yanga ikiwa inajiandaa na mchezo wa ligi pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaitta Dicha FC.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: