Tuesday, 1 May 2018

JACK PEMBA ASUSA MAGARI YA BILIONI 1


Jack pemba (kushoto), akigawa pesa.
BAADA ya kufunguliwa kesi na tajiri mwenzake, Godfrey Kirumira wa nchini Uganda, Pedeshee Jack Marshal Pemba, ametikisa baada ya kuibuka kwa stori kwamba kumbe aliyasusa magari yake matatu ya kifahari yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.2 za Uganda.

Jack Pemba.

Kufuatia habari hizo na nyinginezo huku Jack akihusishwa na video za ngono zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Ijumaa Wikien da lilimtafuta mmoja wa ndugu za tajiri huyo anayejulikana kwa kufanya kufuru ya fedha, Eliudi Pemba ambaye alifunguka kila kitu juu ya sakata hilo.

Magari yake ya kifahari.

Eliudi aliliambia gazeti hili kuwa, ni kweli kwamba, Jack Pemba ambaye anaishi nchini Uganda alimkopa Kirumira kiasi cha dola laki 2 za Kimarekani (zaidi ya shilingi milioni 450 za Kibongo) ambazo mahakama imeamuru kaka yake azilipe, lakini mwenyewe amekataa kwa sababu mdai alivunja makubaliano yao.


Kufuatia msigano huo, wiki iliyopita mahakama iliagiza kukamatwa kwa Jack Pemba ili amlipe Kirumira shilingi bilioni 1 za Uganda kutokana na kukaa na deni lake kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa Eliudi, Jack Pemba alikopa kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Kirumira ambapo alimpa magari yake matatu ya kifahari yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1 za Kitanzania.


Magari yenyewe ni Range Rover lenye pleti namba ya jina la ONLY 1 JP (ikimaanisha kuna Jack Pemba mmoja tu).
Gari hilo linatajwa kuwa na gharama ya dola za Kimarekani 140,000 (zaidi ya shilingi milioni 300 za Kitanzania).
Gari lingine ni Land Cruiser ZX la mwaka 2017 lenye pleti namba ya jina la MR PEMBA ambalo jamaa huyo alilinunua kwa gharama ya dola za Kimarekani 175,000 (karibia shilingi milioni 400 za Kitanzania).
Lingine la kifahari ni Hummer H3 lenye thamani ya dola za Kimarekani 35,000 (zaidi ya shilingi milioni 80 za Kibongo).
Tajiri Godfrey Kirumira.


Eliudi alisema kuwa, kwa fedha za Uganda, jumla ya magari hayo yana gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1.2 za Uganda.
“Walikubaliana yale magari yawekwe hadi atakaporejesha mkopo, lakini alishangaa kuyaona yanatumiwa na jamaa huyo na watoto wake kwa ajili ya matanuzi na kuyakodisha kwa maharusi.
“Alichokisema Jack ni kwamba Kirumira alivunja makubaliano na magari yake yamechakaa hivyo akamsusia,” alisema Eliudi na kuongeza:
“Baada ya hapo ndipo jamaa akaanza figisufigisu za kumchafua Jack kwa kusambaza video za ngono na msichana wa zamani wa Jack ili ionekane kaka yangu ndiye amefanya hivyo.
“Kiukweli sisi kama familia limetuchukiza na kitendo cha kuchafuliwa kwa ndugu yetu na video za ngono maana Jack ana mke hivyo ilikuwa ni kama kumharibia tu na ameapa hatayachukua hayo magari wala kulipa kiasi hicho cha fedha.”

No comments:

Post a Comment