Msanii wa nyimbo za Injili nchini Goodluck Gozbert amefunguka na kusema kuwa kitendo cha kukutana na Rais John Pombe Magufuli na viongozi wengine akiwepo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete inamkumbusha watu ambao walikuwa wakimkatisha tamaa katika kazi yake hiyo.
Goodluck amesema hayo baada ya kupata nafasi ya kwenda Ikulu na kuimba mbele ya viongozi hao katika uzinduzi wa taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation
"Nikukumbushe tu....sikuzaliwa kwenye familia yenye kujulikana au kuwa na heshima kokote kule, na wala sikuwahi kushika hata nafasi ya tano darasani, nakumbuka kuchekwa, kukatishwa tamaa, kuandikiwa ubaya, kunenewa uongo na kutabiriwa kushindwa kila nilipofikiri ningeweza, nakumbuka mengi mengine ya juzi tu. Ila hakuna kitu nakumbuka zaidi kama zile ahadi za Mungu kwangu, hakuna kitu nakumbuka kama huruma za huyu Yesu aliyenipenda nikiwa sijielewi. Kesho nitawaambia wanangu, Mungu aliyenitoa na kunifikisha pale ndiye atakayeenda pamoja nanyi" alisema Goodluck 
Rais Magufuli mara kadhaa alionyesha hisia zake juu ya nyimbo za msanii huyo na kusema kuwa anavutiwa sana hasa zaidi na wimbo wake 'Hauwezi Kushindana' ambao ameutoa miezi  wa tatu mwaka huu. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: