Wafadhili wa kimataifa waliokutana ijumaa mjini Geneva nchini Uswizi wameahidi kiasi cha dola za Marekani milioni mia tano na ishirini na nane za kukabiliana na janga la kibinadamu nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo,Umoja wa mataifa umeeleza.
Kiasi hicho pungufu ya robo ya dola bilioni mbili nukta mbili ambazo umoja wa mataifa ulikadiria kinahitajika mwaka huu kutoa msaada mkubwa kwa wakimbizi ndani ya DRC na wakimbizi wa Congo walioko katika nchi jirani.
Hata hivyo mkuu wa shirika la misaada ya kibinadamu katika umoja wa mataifa Mark Lowcock alisisitiza kuwa matarajio hayakuwa kuchangisha kiasi chote kinachotakiwa katika mkutano huo mmoja.
Alieleza kufarijika na matokeo hayo na kubainisha kuwa mataifa ambayo bado hayajatoa ahadi zao yatafanya hivyo hivi karibuni.
Mkutano huo umefanyika bila ushiriki wa DRC ambayo imegoma kwa kile ilichodai kuwa Umoja wa mataifa unapotosha ukweli kuhusu hali ya kibinadamu nchini mwake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: