Friday, 6 April 2018

DKT. KIKWETE ASEMA VIFO VYA WATOTO WACHANGA VINAWEZA KUZUILIKA, ASIFU JUHUDI ZA CSI


Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya ya taasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI) jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI) jijini Dar es Salaam
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda akitoa  historia ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo, mafanikio na changamoto wakati wa Maadhimisho ya miaka mitano jijini Dar es Salaam
 Mmoja ya waanzilishi wa Childbirth Survival International(CSI), Profesa Taus Kagasheki akitoa shukrani kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kutokana na mchango wake katika kuhakikisha Tanzania tunapunguza vifo vya mama mjazito na mtoto.
 Mshehereshaji kwenye Maadhimisho ya miaka mitano ya tasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI), Babie Kabae akifafanua jambo wakati maadhimisho hayo ambayo yamefanyika jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya waalikwa wakifuatilia hotuba ya rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete wakati maadhimisho ya miaka mitano ya ya tasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI) jijini Dar es Salaam.


RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete amesema matatizo ambayo yanatokana na uzazi yapo ambayo yanaweza kuzuilika na kuhimiza wadau kushirikiana na Serikali kwa lengo la kuendelea kupunguza vifo vya mama mjazito na mtoto.

Pia ametoa pongezi kwa hatua zinazochukuliwa na Taasisi ya Childbirth Survival International(CSI) ya kuhakikisha wanatoa elimu ya afya salama ya uzazi na kushiriki kwa vitendo katika kufanikisha vifo kwa mama na mtoto vinapungua hapa nchini.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya miaka mitano ya CSI na kutumia nafasi hiyo kuwapongeza waanzilishi wa taasisi hiyo Stella Mpanda na Profesa Tausi Kagasheki.

Rais mstaafu Kikwete amesema kumekuwepo na vifo ambavyo vinatokea kwa wajawazito na watoto ambao hawana hatia na kutumia nafasi hiyo kuhimiza wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kupunguza vifo hivyo.

Amesema ipo haja ya kuendelea kutolewa elimu ambayo itasaidia jamii kutambua umuhimu wa kuhudhuria kliniki kwa mama mjazito na kubwa zaidi kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwenye eneo la afya ya uzazi na vifo. Ameelezea hatua ambazo zinachukuliwa katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto.

“Nimefurahi sana kuona taasisi hii imenzishwa na akina mama wa Tanzania. Stella Mpanda yeye ni mkunga na Tausi yeye ni mwanataaluma .Nifaraja sana wamama wa Tanzania kufanya jambo kubwa kama hili la kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza vifo vya wajawazito.

“Wametoa heshima kubwa kwa nchi yetu na pia wamefanya jambo kubwa kwa wanawake nchini kwa kuanzisha taasisi kubwa kama hii ya CSI. Kwa bahati mbaya akina mama wakati mwingine mnashindwa kupongezana. Adui wa mwanamke ni mwanamke ni mwenyewe,”amesema Rais mstaafu Kikwete.

Kuhusu changamoto zilizopo kwenye afya ya uzazi na kwamba moja ya malengo ya milenia inazungumzia kupunguza vifo vya mama mjazito na watoto chini ya miaka mitano.

“ Wakati naingia madarakani mwaka 2005 , vifo kwa watoto wanaokufa ilikuwa 578 kati ya vizazi hai 100,000 wanaozaliwa. Baadae tukapunguza vifo hadi watoto 432 lakini ikapanda tena hadi vifo vya watoto 556 wakati lengo la milenia ilikuwa ni watoto 191.

“Hivyo tukaamua kuweka mikaka katika kuhakikisha tunapunguza vifo hivyo,”amesema.

Hata hivyo takwimu za mwaka 2016 kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni kwamba kati ya vizazi hai 100,000 wanaopoteza maisha ni 556.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: