Wednesday, 4 April 2018

DIAMOND AKANG'ATA MENO MBELE YA HAMISA MOBETO

 
MWANANA Hamisa Mobeto ameibua gumzo wakati wa utoaji wa tuzo za Sinema Zetu baada ya kuamua kumtaja msanii maarufu Nassib Abdul a.k.a Diamond Platnumz ndio amemvutia zaidi kwa wageni waliofika kwenye sherehe hizo za utoaji tuzo.

Jina la Mobeto si geni kwa Watanzania walio wengi na hasa wanaofuatilia maisha ya mastaa wa kibongo na umaarufu wake uliongzeka zaidi baada ya kubainika amezaa na Diamond.

Usiku wa jana Mobeto alikuwa moja ya wageni waalikwa katika utoaji wa tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Azam TV kupitia chaneli ya Sinema Zetu.Ndani ya ukumbi huo alikuwepo na Diamond.

Wakati mambo yakiendelea ukumbini hapo ndipo moja ya washehereshaji alipoamua kumfuata Hamisa Mobeto na kisha kumuuliza ni nani ambaye anaona amependeza ukumbini hapo kuliko mtu mwingine yeyote na anafurahia uwepo wake.

Jibu la Hamisa Mobeto bila kuchelewa akataja jina la Diamond.Wakati anaaza kuulizwa Diamond alikuwa anasikilizia kwa umakini mkubwa na baada ya kutajwa yeye akajikuta aking'ata meno kwa nguvu na kwa muda wa zaidi ya dakika tatu akiwa ameshika kichwa chake.

Hata hivyo ukumbini hapo wageni waalikwa walilipuka kwa shangwe kwa kupiga kelele.Wakati Hamisa akimtaja Diamond, Wema Sepetu aliyekuwepo eneo hilo yeye alionekana akiwa 'bize' na kuchati kwenye simu yake ingawa sura yake ilionekana kutofurahia.

Ilipofika muda wa kutoa zawadi kwa moja ya washindi wa tuzo hizo akaitwa tena Diamond na Hamisa Mobeto wapande jukwaani kutoa tunzo.Hali hiyo ikamfanya Diamond kukosa la kufanya.

Hivyo akatumia nafasi hiyo kupongeza Azam TV kwa kuandaa tuzo hizo kwani zimewakutanisha wasanii mbalimbali na hata yeye amepata nafasi ya kukutana na mzazi mwenzie(Hamisa) na kufafanua hata mtoto wao akiona atafurahia kuona wakiwa wawili jukwaani hapo.

No comments:

Post a Comment