Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando akikagua ujenzi vya vyumba vya madarasa


Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi  Salehe  Mhando ameunga mkono jitihada za wananchi wa Kijiji cha Luhafwe ambao wameanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa  ya shule ya msingi Ruhafwe iliyopo wilayani humo kwa kuchangia Sh.Milioni moja.

Ujenzi huo unatekelezwa kwa nguvu na  wananchi na uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha pamoja na Mkuu wa Wilaya kilichofanyika katika kijiji hicho.

Katika mazungumzo yake na wananchi wa Kijiji hicho  Mhando amesema wananchi wameguswa kwa sejemj kubwa na suala la huduma za jamii katika eneo hilo na kujitolea kwa hali na mali huku akieleza kuwa kiasiwa cha shilingi milioni sita tasilimu zimetolewa  na  wananchi hao.

“Niwashukuru sana wananchi wa Luhafwe kwa ushirikiano walio uonyesha katika uanzishwaji wa ujenzi wa hii shule eneo hili la Luhafwe lilikuwa halija rasimishwa na sasa kwa jitihada za halmashauri na serikali kwa ujumla baada ya kulikubali hilo na ndio maana sasa tunakuja na uanzishwaji wa huduma za kijamii “alisema Mhando.

Katika hatua nyingine,Mkuu huyo  amesema ni wajibu wa kila mwananchi kushiliki katika shughuli za maendeleo ya kijijiji hicho ili kutatua tatizo la ukosefu wa miundo mbinu mbali mbali kama vile afya pamoja na elimu.

Mhando ameongeza kusema kuwa serikali ya awamu ya tano kupitia mradi wa Equip imeunga mkono jitihada za wananchi kwa kupeleka kiasi cha Tsh mil 60.5 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa,ofisi moja ya walimu na ujenzi wa vyoo.

Awali eneo hili la Luhafwe halikuwa eneo rasmi la makazi lakin kwa sasa eneo hilo lililopo katika eneo la uwekezaji la halmashauri limerasmishwa rasmi kuwa eneo la makazi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: