Sunday, 15 April 2018

DC Kasesela atoa ujumbe mzito kwa Vijana


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela amewataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ili ziweze kuwanufaisha.

Ameyasema katika Tamasha la Amka Vijana la Wasanii wa filamu nchini lililofanyika katika viwanja vya Mwembe Togwa mkoani humo.

Msanii wa muziki wa singeli, Dulla Makabila alikuwa mmoja kati ya wasanii waliofanya vizuri hali iliyomfanya DC. Kasesela kuinuka na kuanza kuonyesha uwezo wake wakucheza singeli jukwaani.

Katika tamasha hilo lililofanyika hapo jana lilikuwa na lengo la kuhamasisha vijana kujishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ili wawewze kujipatia kipato.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela amewataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo za kimaendeleo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: