CHIKOKA AFUNGUKIA MAANDAMANO! - MSUMBA NEWS BLOG

Thursday, 5 April 2018

CHIKOKA AFUNGUKIA MAANDAMANO!


MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Juma Chikoka, amesema kuna tatizo kubwa la uelewa wa Watanzania katika suala zima la matumizi ya mitandao ya kijamii hali inayowasababisha wengine wafuate mkumbo wa maandamano yasiyokuwa na tija.

Chikoka alisema tatizo kubwa ni mitazamo ya vijana na watumiaji wengi wa mitandao kwamba imekuwa ya kawaida au hasi.

“Mtu hafikiri nje ya boksi namna ya kutumia mitandao kujiongezea kipato. Yaani asubuhi anangalia nani kamsema nani, mchana nani kamchamba nani naye ashabikie, jioni wapi kuna bata. Ndiyo hao wanaofuata upepo hata wa kutangaza maandamano bila hata kujua yanahusu nini,” alisema Chikoka.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done