Monday, 2 April 2018

Chelsea, Arsenal zapoteza matumaini ya kusalia ‘Big Four’ EPL

Klabu ya Chelsea imepoteza mchezo wake wa raundi ya 31 ya Ligi Kuu Uingereza (EPL) dhidi ya Spurs kunako dimba la Stamford Bridge matokeo ambayo yameifanya klabu hiyo kupoteza matumaini ya kusalia kwenye nafasi nne za juu za EPL ili kushiriki michuano ya klabu bingwa msimu ujao.
Chelsea imepoteza mchezo huo kwa kipigo cha goli 3-1. Magoli ya Spurs yamefungwa na Christian Eriksen na Dele Alli x2 huku goli la Chelsea likifungwa na Alvaro Morata.
Matokeo mengine ni Arsenal wameibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Stoke City ambapo hata hivyo licha ya ushindi huo bado Arsenal wapo nafasi ya sita.
Chelsea na Arsenal zipo nafasi ya tano na sita kwenye msimamo wa EPL huku zikiwa zimeachwa na Spurs alama zaidi ya nane  na zikiwa na michezo 7 mkononi.
Ushindi wa leo wa Spurs unazifanya klabu ya Chelsea na Arsenal kupoteza matumaini ya kuingia Big Four kwani umeongeza gepu la pointi.

No comments:

Post a comment