Saturday, 14 April 2018

Breaking News : Polisi Wadaiwa Kupigana Risasi Tanga


ASKARI Polisi waliokuwa lindoni katika Benki ya CRDB Tawi la Tanga Mjini wanadaiwa kupigana risasi leo Jumamosi, Aprili 14, 2018na kusababisha kifo cha mwenzao mmoja, hata hivyo, majina yao hayajafahamika mara moja.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, inadaiwa kwamba, mmoja wa askari hao alimpiga risasi mwenzake na kumjeruhi mguuni hivyo akawa kama amepagawa na kuanza kufyatua risasi hovyo. Inadaiwa pia kwamba chanzo cha ugomvi huo ni tuhuma za wivu wa mapenzi.

Wakati tukio hilo likitokea inadaiwa askari wengine walikuwa eneo la jilani wakifanya mazoezi hivyo baada ya kuona mtu akirusha risasi hovyo walihisi ni mhalifu hivyo wakamfyatulia risasi iliyompata kichwani na kupoteza maisha.

Aidha, Mtandao huu  ulimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Michael Wakulyamba ambaye amesema hajatapata taarifa za tukio hilo kwani yupo safarini hivyo anafuatilia ili kufahamu iwapo ni kweli limetokea na mazingira ya tukio yalikuwaje.
Taarifa zaidi tutaendelea kufuatilia, tutakujuza.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: