Monday, 9 April 2018

ASKOFU KAKOBE AJISALIMISHA UHAMIAJI SAKATA LA URAIA WAKE


Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe amefika katika Ofisi za Uhamiaji Makao Makuu jijini Dar es Salaam zilizopo Kurasini kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni mashaka juu ya uraia wake kufuatia barua aliyoandikiwa na Mamlaka hiyo Aprili 5, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika ofisi hizo, kakobe amesema kuwa lengo kuu lilikuwa juu ya uraia wake ambapo amewaeleza kuwa yeye ni Raia wa Tanzania na mzaliwa wa Kijiji cha Kibilizi wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Kakobe amesema ameulizwa pia juu ya cheti cha kuzaliwa na akawambia enzi za kuzaliwa kwake mwaka 1955 vyeti hivyo vilikuwa havitolewi kwani harakati za kuanza kutolewa vyeti vya kuzaliwa zilianza mwaka 1981 hivyo akasema kama watahitaji zaidi ya ukoo wake wafike Kijiji cha Kanyonza kilichopo Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Akizungumza wakati wa mahubiri yake jana, Askofu huyo alisema hatikiswi na upepo unaotikisa nyasi. huku nakiwaasa waumini wake wasimame imara kila wanapokumbana na changamoto na kuongeza kuwa hana hofu kwani wokovu wake siyo wa dhahabu bandia

No comments:

Post a comment