WAZIRI wa Mambo ya ndani, Dk  Mwigulu Nchemba amewataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na inapobidi matumizi ya fimbo yatumike.

Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari  Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida, jana, Dk Nchemba alisema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi ili kutengeneza hatma ya nchi.

"Kuna wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi lakini ninyi hamuoni hii na kulalamika tu, kinachofanyika ni kwa manufaa yetu...niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo ili kutengeneza taswira ya nchi yetu," alisema Dk Mwigulu.


Alisisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa.


Alisema ni majengo ya taasisi yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.


"Naunga mkono ujenzi huu wa mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu hivyo nachangia mifuko 200 ya saruji nawaahidi pia kutoa Sh milioni sita," alieleza.


Mkuu wa Wilaya Iramba, Emmanuel Luhaula alisema shule higo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma kutokana na umahiri wa walimu kwani watoto hao wanajua kujieleza kama vile wanasoma chuo kikuu.


Alisema wananchi wa Iramba wanatakiwa kujivunia  kuwa na shule zao pamoja na walimu hao ili kuboresha elimu wilayani humo.


"Unafanya jitihada ili kuhakikisha kila sekondari kunajengwa mabweni ili kuondoa kero za wanafunzi.Sisi wa Iramba tushindwe wenyewe kukutumia. Nimekuwa Mbunge lakini anayoyafanya mbunge huyu Mimi sikuyafanya," alisema Luhaula.


Naye, Mkuu wa shule hiyo, Jeremiah Kitiku alisema licha ya kufanya vizuri kitaaluma, wanakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa baadhi ya majengo, upungufu vitabu vya masomo ya kiada 274.


"Mahitaji ya vitabu vya kiada no 2,802 vilivyopo 2,328 upungufu ni 274. Pia tunachangamoto ya kutokuwa na uzio kwa usalama wa wanafunzi, walimu na mali za shule," alisema Kitiku

Hata hivyo, alisema malengo ya shule hiyo ni ukarabati wa vyumba tisa vya madarasa na  ofisi za nane za walimu ambazo zitagharimu Sh Milioni 169.4.


Katika harambee hiyo, saruji iliyokusanywa ni mifuko 209, ahadi  ya fedha ni 8,486,000, ahadi ya mifuko ya saruji 572, Gypsum 50 na  nondo tani moja jumla ya ahadi na fedha taslimu ni 19,494,300
Share To:

msumbanews

Post A Comment: