TAKUKURU yazitaja Halmashauri za Arusha Kuongoza kwa Rushwa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Arusha imezitaja Halmashauri za mkoa wa Arusha kuwa inaongoza kwa rushwa katika kipindi cha miezi sita kuanzia July 17, 2017 hadi December 17, 2017 na kuongeza kwamba wameweza kuokoa Tshs Milioni Thelathini na tano na laki sita ikiwa ni ya mishahara hewa.
Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha Frida Wikesy amesema idara nyingine iliyoongoza ni pamoja na sekta ya utalii ikifuatiwa na ile huduma za kijamii.
Ameongeza kuwa wamekuwa na kesi thelathini na tatu ambapo wameshinda kesi tatu huku nyingine zikiwa zinaendelea mahakamani.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: