SIMBA YAPATA PIGO KLABU, MFANYAKAZI WAKE AFARIKI GHAFLA
Klabu ya Simba imepata pigo baada ya katibu mukhtasi wake kufariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo.

Julliet alikuwa ni mfanyakazi wa klabu hiyo katika ofisi za makao makuu yake Barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amethibitisha kutokea kwa msiba wa Julliet ambaye inaelezwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: