Simba kuweka kambi Iringa kuwawinda Njombe Mji

Simba SC wameondoka asubuhi ya leo majira ya saa moja kuelekea Iringa kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya safari ya Njombe kwa ajili ya mchezo wa ligi.

Kikosi hicho kitaweka kambi Iringa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na Njombe Mji kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara.

Mechi hiyo ya ligi, itachezwa Aprili 3 2018 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe huku wenyeji wakiwa wametoka kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la FA dhidi ya Stand United jana.

Wekundu hao wa Msimbazi wataondoka Iringa Jumatatu ya wiki lijalo kuelekea Njombe, tayari kwa mchezo huo utakaopigwa siku ya Jumanne
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: