Muda wowote kolabo ya Alikiba na Yvonne Chaka Chaka inatoka

Mashabiki wamekuwa na shauku ya kutaka kujua iwapo kolabo ya Alikiba na mwanamuziki mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka ipo mbioni kutoka.

Hii ni baada ya Yvonne Chaka Chaka kuposti katika ukurasa wake wa Instagram ujumbe alioandikiwa na Alikiba, ujumbe huo ulisema; I love you Mom Chacha Chaka. Baada ya ujumbe huo Yvonne Chaka Chaka akajibu; I love you back my son.

July mwaka jana Alikiba alipoulizwa kuhusu kolabo yake na Yvonne Chaka Chaka alijibu; Kiufupi kwamba wimbo upo na taratibu tulishafanya kama mlivyoona tupo studio lakini kuna ratiba lazima ziwepo sio tu umefanya halafu unatoa. Kuna mipango tupo nayo tayari na kila nyimbo itatoka kwa muda wake.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: