MBOWE NA WENZAKE WAPELEKWA MAHABUSU SEGEREAMwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano wa chama hicho wamepelekwa katika mahabusu ya Segerea baada ya kunyimwa dhamana katika kesi yao waliyosomewa leo Katika Mahakama ya Kisutu Dar.

Mbowe na wenzake wamefikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashtaka manane ikiwemo kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilina Akwiline, Feb 16 mwaka huu, uasi na kuhamasisha chuki.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, washtakiwa wote walikana ambapo Wakili Nchimbi alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

Pia, Nchimbi aliwasilisha maombi kwa mahakama hiyo ili washtakiwa wasipewe dhamana kwa sababu ya usalama wa umma wa Watanzania ambapo washtakiwa walipelekwa Segerea na kesi yao itaendelea tena Machi 29, mwaka huu.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: