Wednesday, 14 March 2018

Man United watupwa nje na sevilla

Sevilla wakifurahia ushindi
Klabu ya Manchester United imeyaaga mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Sevilla kutoka Hispania.
Sevilla ndio walikuwa wa Kwanza kupata goli kunako dakika ya 73 na 78 kupitia kwa Ben Yedder huku goli la Man United la kufutia machozi likifungwa na Lukaku.
Baada ya mchezo huo, Kocha Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa ameyapokea matokeo kwa furaha ingawaje wachezaji wake wanamajonzi.
“Ni kweli Kila mtu ana huzuni lakini Mimi nimepokea matokea kwa furaha katika kipindi ambacho wachezaji wote wamejawa na huzuni. Kwani baada ya ushindi wa Liverpool niliwambia wachezaji kuwa kila mechi inayokuja ni lazima tushinde ili tusonge mbele walijua hilo, na kwa Sasa tufikirie zaidi mechi zinazokuja matokeo hayawezi kubadilika,”amesema Mourinho kupitia mtandao wa klabu ya Man United usiku wa Jana baada ya mchezo kumalizika.

No comments:

Post a comment