Picha ya Maktaba

Ofisa Tarafa wa Kibamba, wilayani Ubungo, Beatrice Mbawala amejifungua watoto wanne kwa mpigo katika Hospitali ya Agha Khan, jijini hapa.
Beatrice amejifungua watoto hao wakiwa njiti mwezi mmoja uliopita.
Akizungumza hospitalini hapo, leo Machi 3, baba wa watoto hao, Julius Mbawalla amesema familia yake ina furaha kupokea watoto wanne na kwamba jukumu lake kubwa ni kuhakikisha mkewe anapata huduma muhimu ili aweze kumudu kuwanyonyesha.
Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali ya Agha Khan, Dk Mariam Mgonja amesema afya za watoto zimeimarika na tayari wameruhusiwa kwenda nyumbani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: