Mabasi ya Mwendokasi yarejesha safari zake


Kampuni ya Mabasi ya Mwendokasi jijini Dar es salaa (UDART) imerejesha tena barabarani huduma yao baada ya kusitisha huduma ya usafiri kwa muda.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART,Deus Bugaywa amesema kuwa wanaomba radhi kwa wananchi wote wanaotumia usafiri huo .

“Tunapenda kuujulisha umma  kwamba huduma za mabasi hayo zimerejea kuanzia saa 3:00 asubuhi baada ya kusitishwa kwa muda tangu saa 11:00 alfajiri’’amesema Buganywa.

Mapema leo alfajiri, huduma ya usafiri wa mabasi ya mwendokasi ilisitishwa  kutokana kufungwa kwa Barabara ya Morogoro katika eneo la Jangwani kufuatia mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

Leo asubuhi katika barabara zote kuu jijini Dar es salaam kulikuwa na foleni kubwa ambapo hadi kufikia saa nne ya asubuhi bado barabara zilikuwa hazijafunguka.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: