Sunday, 18 March 2018

Kituo kikubwa cha runinga duniani chatoa pongezi kwa Diamond Platnumz

Kituo cha runinga cha kimataifa cha ‘BET ‘ kimetoa pongezi kwa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz baada ya album yake mpya ya ‘A Boy From Tandale’ kuingiza nyimbo tano zinazosikilizwa zaidi kwenye mtandao was iTunes nchini Burkina Faso.
Kituo hicho kimetoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika |”Hongera Diamond Platnumz kwa kuingiza nyimbo tano zinazosikilizwa zaidi nchini Burkina Faso kwenye mtandao wa iTunes”.
Jumatano Machi 14, 2018 Diamond Platnumz alizindua album hiyo jijini Nairobi nchini Kenya.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: