Jerry Muro alivyotinga kuwasapoti Simba Taifa


Katika hali ambayo siyo ya kawaida sana kuiona Tanzania ni kuona Shabiki wa Simba akishangilia Yanga au shabiki wa Yanga akishangilia Simba.

Katika Mchezo kati ya Simba na Al Masry uliochezwa jana aliyewahi kuwa msemaji wa Yanga Jerry Muro alitinga uwanjani kuisapoti Simba lakini akiwa na Uzi wake wa Yanga.

Imekuwa ni kazi Ngumu kwenda kwenye mechi kama hizo na jezi ya Yanga na uruhusiwe na washabiki wa Timu pinzani kukaa na jezi yako lakini kwa Jerry ilikuwa Tofauti kwani alikaa akiwa na Scarf ya Simba kwenye jukwaa la Simba huku akiwa amevaa uzi wa Yanga.

Jerry  kupitia Ukurasa wake wa Instagram pia hakuishia kukaa hivi hivi alitupia Ujumbe wake huku akisisitiza watu kuwa wazalendo hasa linapokuja suala la Kitaifa watu.
Ujumbe wa Jerry Muro Huu hapa.

Uzalendo ni Imani na Msingi wa Umoja na Mshikamano wetu, Mpira unatuleta pamoja Watanzania tusiruhusu Ushabiki Uondoe Uzalendo wetu katika Mambo Makubwa ya Kimataifa, Hongera Swahiba sio Haba @hajismanara#MzalendoHalisi #UmojaWetu

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: