Zahanati ya Kata ya Majengo Katika Halmashauri ya Meru Mkoani Arusha Imezungukwa na maji pande zote nne baada ya mvua zinzoendelea kunyesha, Hali inayopelekea wananchi kukosa huduma za Afya katika Zahanati hiyo.


Akizungmza na Msumbanews Blog wananchi wa Kata hiyo wameeleza kuwa
 "Hili tatizo ni la muda mrefu tokea huwa linajirudia kwa kila mwaka hususani kipindi hiki cha Masika tokea mwaka 1988, na hali hii usababishwa na mikondo ya maji ambayo hupita karibu na hospital hii tumejaribu kuzuia kwa kuchimba mitaro kwa kushirikiana na Serikali hata mwaka jana Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo alipokuwa kwenye ziara yake katika Kata hii tulimueleza kero hii na akaagiza wakandarasi wakaja kutuchimbia mitaro, Lakini mtaro ule haukusaidia chochote kwani walichimbaa mdogo sana na ukashindwa kuzuia kasi ya haya maji ndio maana yamerudi tena mwaka huu hadi wauguzi wetu wameamua kujipa likizo maana kila wakija zahanati imezungukwa na maji hakuna pakuingilia na sisi inabidi tukajitibu kwenye zahanati za jirani."

Kilio cha wananchi hao kiliwafikia Viongozi wa chama cha Mapinduzi kwa kushirikiana na viongozi Afya Wilaya wakafunga safari hadi eneo la tukio kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo na kupelekea kutoa maamuzi ya muda mfupi na mrefu.

Maamuzi yaliyotolewa ni kuwa Jengo la mtendaji wa kata litumike kutoa huduma ya Afya kwa kipindi ambacho mvua zinaendelea kunyesha, Mwakilishi wa Afisa Afya wa Wilaya Dkt.Amani Mlay alikagua na kuridhishwa na jengo hilo na kumwagiza Mtendaji Kata zoezi la kuhamishia Zahanati hiyo katika majengo hayo lianze mara moja ili wananchi waendelee kupata huduma za Afya kama kawaida huku maamuzi ya muda mrefu ya kuihamisha Zahanati hiyo katika eneo hilo yakishuhulikiwa.


Hii ni nyumba ya daktari wa Zahanati hii baada ya mvua kubwa zinmzoendelea kunyesha ameamua kuhama hapa.

Kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Ndg. Remmy Naasary na Katibu Uvccm kata ya Majengo Ephraem Mollel wameipongeza na kuishukuru serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua wanazozichukua kutatua matatizoya wananchi kwa haraka hasa katika huduma zamuhimu kama Afya .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: