Thursday, 1 March 2018

Davido afunguka sababu za kumtaja Ronaldo mara kwa mara kwenye nyimbo zake


Staa wa Muziki kutoka nchini Nigeria David Adedeji Adeleke maarufu kwa jina la ‘Davido’ amesema kuwa yeye pamoja na Cristiano Ronaldo ambaye ni Staa wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno ni Marafiki.
Staa huyo ambaye anafanya vizuri kwa sasa katika Soko la Muziki Afrika na Duniani kwa ujumla amesema hayo wakati akihojiwa na Moja kati Website maarufu ya Michezo ya ‘Goal’. Davido amesema kuwa hawajawai kukutana kutokana na wawili hao kuwa bize na shughuli zao za kila siku ingawa amesema kuwa ana Mpango wa kufanya Video na Staa huyo ambayo haitakuwa kwa ajili ya Wimbo ila atafikiriwa kipi watakifanya.

No comments:

Post a Comment