Daraja la Kivule lililopo eneo la Sirari Wilaya ya Ilala limekatika kutokana na mvua zilizoanza kunyesha leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wetu ameshuhudia msururu wa watu wakishindwa kupita kwenye daraja hilo huku wakitafuta njia mbadala.
Daraja hilo lilikatika baada ya kuzolewa na mvua kubwa iliyonyesha leo kuanzia asubuhi mpaka mchana.
Magari yote yanayoelekea Kivule yalishindwa kupita yakiwemo ya abiria yaliyolazimika kuishia Mwembeni.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: