Wednesday, 7 March 2018

Baba mdogo Nondo Mwanangu arudishwe akiwa mzima


Familia ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imefunguka na kuwataka watu ambao wamemteka mwanafunzi huyo kuhakikisha anamrejesha akiwa mzima.
Baba mdogo wa Abdul Nondo amesema hayo leo Machi 7, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kipindi ambacho viongozi wa mtandao huo wa wanafunzi wakitoa rai yao kwa jeshi la polisi kuhusu kupotea kwa mwenzao. 
"Abdul ni kijana mdogo mno na amewahi kutuambia mara kwa mara kuhusu vitisho ambavyo amekuwa akivipata lakini hatuna nguvu kusema kuwa tutamkinga vipi. Sisi kama familia tunaomba kijana arudi akiwa mzima maana ana ndoto zake, mama yake saizi mgonjwa anaumwa pressure baba yake pia. Huyu Nondo ana ndoto zake kama mtoto pia ana ndoto zake kama mwanafunzi atatimiza vipi, sisi kama familia bado tunaendelea kulaani na tunavuta subira katika hili kwamba huenda akapatikana tunachoomba aje salama asije akarudi hana mkono akashindwa kusonga na kumsaidia mama yake" alisema baba mdogo wa Abdul 
Baba mdogo wa Abdul aliendelea kusema 
"Hatujui alipo lakini kama yupo kwa wale ambao tunawasikia kila siku maanake wanajulikana tunaomba arudi huyu kijana maisha yake na historia yake ni ngumu wamrudishe huyu kijana anatafuta njia hana kingine anachokitafuta pale, kuongea sana vile au kujionyesha sana vile na uwezo wa kufanya ikiwa pamoja na kusoma sana vitabu anafanya vile kutafuta kuing'arisha ndoto yake itimie hivyo wamuache aje akamilishe ndoto yake" 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: