Sunday, 25 February 2018

Zijue mbinu Za kujitibu chunusi Bila Kutumia Na Gharama Kubwa


Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni. Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bakteria.

Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris. Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17.

Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe (adolescents).

Hivyo zifuatazo ni mbinu za kujitibu chunusi;

1.   Asali:
Matumizi ya asali kutibu chunusi huwezesha ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.

Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.

 2. Limao
Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwenye maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha acha pakauke, unaweza kurudia rudia kila baada ya masaa kadhaa.
Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa (ya dukani), kwa sababu yanaweza kuwa yamewekwa kemikali zingine ili kuyahifadhi kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao halisi.

3. Dawa Ya Meno:
Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanya kazi vizuri.

Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au ngano iliyosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10. Lakini pia safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

 4. Papai:
Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.

Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na upakae sehemu yenye chunusi, kisha liache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kujisafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.

5. Mvuke:
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo huku ukielekeza uso wako kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke kwa dakika 5 mpaka 10 hivi. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.

6. Poda:
Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na kuiacha mpaka asubuhi.

MHIMU: Kunywa maji ya kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10, jishughulishe na mazoezi ya viungo na ujiweke msafi kila mara.

Njia hizi za Asili zinaweza kuchukuwa muda kidogo mpaka kuona matokeo ya kuridhisha. Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali iliyo karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: