Serikali imeonesha kushitushwa na bajeti ya Milioni 80 iliyotolewa  na familia ya marehmu Akwelina kwa ajili ya mazishi ya mpendwa wao Akwelina.

Msemaji wa familia hiyo,Festo kavishe amesema mara baada ya bajeti hiyo kuiwasilisha upande wa serikali ambayo ilijitishwa jukumu la kugharamia mazishi hayo imeonesha kushangaa kwa kuona mzigo mkubwa.

"Katibu mkuu na mkuu wa wilaya walipoiangalia bajeti yetu wakasema kwa nini mmeweka mzigo mkubwa namna hii"  .Festo kavishe

Festo amesema  walimwambia katibu mkuu kwamba hiyo ni bajeti iliyojadiliwa na familia.hawaangalii pesa, wanachotaka  ni matukio halisi yaliyowekwa kwenye bajeti hiyo yafanikiwe.

"wao wametuambia wanaweza kupata jeneza na vitu vingine kwa bei nafuu" 

"Sisi hatuangalii pesa,tunaangalia vitendea kazi ndani ya bajeti.tulichomwambia katibu mkuu kama wao wataweza kutuletea vifaa hivyo tulivyoorodhesha itakuwa vizuri".Alisema Festo.

Festo amesema baada ya mazungumzo marefu serikali iliona uhalisia wa bajeti hiyo na kukubali kutoa kiasi hicho cha pesa.

Akwelina alipigwa risasi akiwa kwenye daladala  kutokana na vurugu zilizotea baina ya wafuasi wa CHADEMA na polisi katika eneo la Kinondoni Dar es salaam.Mwili wake utaagwa siku ya Alhamisi katika viwanja vya chuo cha NIT alikokuwa anasoma na kusafirishwa kueleka Moshi ambako atapumzishwa katika nyumba ya milele siku ya ijumaa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: