Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Februari, 2018 saa 3:00 asubuhi atawaapisha Mabalozi wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa watakaoapishwa ni Mhe. Muhidin Ally Mboweto ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Mhe. Dkt. Wilbrod Peter Slaa ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.
Kwa taarifa kamili soma hapa chini
Share To:

msumbanews

Post A Comment: