Wednesday, 28 February 2018

Picha: Barakah The Prince na mpenzi wake Naj, kama zamani


Baada ya kutoonekana pamoja kwa kipindi kirefu hasa kwenye mitandao ya kijamii, Barakah The Prince na mpenzi wake Naj wameanza kuonekana tena pamoja kama ilivyokuwa hapo awali.
Barakah na Naj wamekutana nchini Uingereza ambapo Barakah alienda kufanya show ya Valentines Month Party pamoja na Rayvanny na Zari The Boss Lady.
Pia katika party hiyo iliyofanyika weekend iliyopita Naj alihusika katika upande wa Special appearance baada ya hapo mahaba ya wawili hao yakaendelea.Hivi karibuni kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM Barakah The Prince aliulizwa kuhusu kufunga ndoa na Naji na jibu lake lilikuwa;
“Tuna mipango mingi sana, sema ni person sana siwezi kuvizungumzia lakini tuna mipango mingi ya kimaisha, vitu vingine unakuwa unamuachia Mungu, sio kwamba ukiwa na mipango ndio inaweza ikatimia,” alisema Barakah.

No comments:

Post a comment